Afisa Utawala

Kategoria:

Muhtasari wa Kazi

Afisa Utawala Bora atatoa usaidizi wa kiufundi katika kuimarisha mifumo na taasisi za utawala bora wa maliasili katika ngazi za jamii na serikali za mitaa. Nafasi hii isratibu na kuwezesha afua zinazolenga kukuza utawala wa misitu, ardhi, wanyamapori na maliasili nyinginezo ulio wa wazi, unaowajibika, unaoshirikisha wote, na wenye ufanisi ndani ya maeneo ya mradi. Afisa ataimarisha uwezo wa halmashauri za vijiji, Kamati za Maliasili za Vijiji (VNRCs), Wasimamizi wa Misitu wa Vijiji (VFMs), kata, na wadau wengine husika kuhusu utawala bora wa maliasili, sera, sheria, kanuni, uwajibikaji, na haki za jamii.

Nafasi hii pia itasaidia kuzuia na kutatua migogoro kwa njia ya ushirikikaji, mifumo ya kushughulikia kero, ugawaji wa faida kwa usawa, na ushirikishwaji wa maana wa wanawake, ikifanya kazi kwa karibu na jamii, vijana, na makundi yaliyo hatarini katika ufanyaji wa maamuzi kuhusu maliasili. Afisa atafanya kazi kwa karibu na jamii, mamlaka za serikali za mitaa, washirika wa uhifadhi, na timu za mradi ili kuboresha utendaji wa taasisi, uzingatiaji wa sheria, uwajibikaji, na umiliki wa jamii katika mipango endelevu ya usimamizi wa maliasili.

Majukumu na Kazi za Msingi:
Majukumu kuu yatajumuisha, lakini si tu:

  • Kuratibu shughuli za utawala bora wa maliasili katika ngazi za jamii, kijiji, kata, na wilaya ili kuimarisha usimamizi endelevu na unaowajibika wa misitu, wanyamapori, ardhi, na maliasili nyinginezo.
  • Kuimarisha taasisi za jamii za utawala bora wa maliasili, ikiwa ni pamoja na Halmashauri za Vijiji (VCs), Kamati za Maliasili za Vijiji (VNRCs), Wasimamizi wa Misitu wa Vijiji (VFMs), serikali za vijiji, na vyombo vingine husika vya jamii.
  • Kuwezesha ujengaji wa uwezo kwa wajumbe wa Halmashauri za Vijiji, VNRCs, VFMs, na wadau wengine kuhusu utawala bora wa maliasili, wajibu na majukumu, sera husika, sheria, kanuni, na mifumo ya uwajibikaji.
  • Kuhamasisha matumizi ya kadi za matokeo (scorecards) ili kufuatilia utendaji, kupima maendeleo, na kuboresha uwajibikaji kwa kubadilisha data kuwa vipimo vilivyo wazi. Kukuza uwazi na uwajibikaji katika ufikiaji, usimamizi, na matumizi ya maliasili, ikiwa ni pamoja na mapato ya maliasili ya jamii, faida, fedha za uhifadhi, na rasilimali nyingine zinazofadhiliwa na mradi.
  • Kuwezesha mazungumzo ya utawala bora na ushirikishwaji wa wadau miongoni mwa jamii, mamlaka za serikali za mitaa, viongozi wa kimila/jamii, wadau wa uhifadhi, na wadau wengine husika ili kutatua changamoto na migogoro ya usimamizi wa maliasili.
  • Kusaidia uundaji, kuimarishwa, na utekelezaji wa mifumo ya utawala ya jamii, sheria ndogo, kanuni, mipango ya usimamizi, na taratibu za kitaasisi kwa ajili ya usimamizi endelevu wa maliasili.
  • Kufuatilia utendaji wa utawala bora wa taasisi za jamii za usimamizi wa maliasili na kubaini pengo, hatari, na fursa za kuimarisha ufanisi wa taasisi na uwajibikaji.
  • Kuhamasisha ugawaji wa faida kwa usawa kutokana na maliasili na jitihada za uhifadhi, kuhakikisha kuwa faida na fursa zinapatikana kwa jamii na kugawanywa kwa haki miongoni mwa makundi mbalimbali ya kijamii.
  • Kusaidia kuzuia na kutatua migogoro inayohusiana na ardhi, misitu, wanyamapori, ufikiaji wa maliasili, matumizi ya rasilimali, na utekelezaji wa shughuli za uhifadhi.
  • Kuimarisha uelewa wa jamii kuhusu haki za ardhi na maliasili, wajibu, sheria husika, kanuni, na mifumo ya kuripoti ukiukwaji au kero.
  • Kuanzisha na kuimarisha mifumo ya kushughulikia kero na marejesho inayowawezesha wajumbe wa jamii na wadau wengine kuwasilisha changamoto kwa usalama, kutoa marejesho, na kutafuta suluhu ya kero zinazohusiana na mradi au usimamizi wa maliasili.
  • Kuhamasisha utawala bora unaozingatia jinsia na ujumuishaji wa kijamii, ukihakikisha uwakilishi na ushirikishwaji wa sawa wa wanawake, vijana, makundi yaliyotengwa, na makundi mengine yaliyo hatarini katika ufanyaji wa maamuzi ya maliasili.
  • Kushirikiana na vyombo vya usimamizi wa sheria na mamlaka husika ili kuimarisha uelewa wa jamii, uripotaji, na utii wa sheria na kanuni za usimamizi wa maliasili, huku ikihifadhii mipaka na majukumu sahihi ya kitaasisi.
  • Kuandika masomo ya utawala bora, mbinu bora, changamoto, na hadithi za mafanikio na kuwezesha ujifunzaji miongoni mwa jamii, mamlaka za serikali, na wadau wa mradi.
  • Kuandaa mipango kazi ya mwaka na robo mwaka, bajeti, taarifa za maendeleo, na nyaraka nyingine zinazohusiana na utawala bora kulingana na mahitaji ya mradi na sera za shirika.
  • Kutenda kazi nyingine yoyote husika kama itakavyopangiwa au kukabidhiwa na uongozi wa mradi.
Sifa za Chini za Kazi na Mahitaji Mengine:
Sifa za chini za elimu na mahitaji mengine yatajumuisha, lakini si tu:

  • Uwe Mwenye Shahada ya Kwanza (Bachelor's Degree) ya Utawala Bora, Masomo ya Maendeleo, Usimamizi wa Miradi, Usimamizi wa Maliasili, au fani zinazohusiana; Shahada ya Uzamili (Master's degree) ni sifa ya ziada.
  • Angalau miaka mitano (5) ya tajriba ya kazi katika fani hii.
  • Ufahamu na tajriba ya awali katika kufanya kazi na miradi ya uhifadhi na usimamizi endelevu wa maliasili ni sifa ya ziada.
  • Tajriba iliyothibitishwa ya kufanya kazi katika maeneo ya vijijini na yaliyojitenga nchini Tanzania ukifanya kazi na serikali za mitaa, VNRCs, Wasimamizi wa Misitu wa Vijiji, katika kutekeleza miradi ya maendeleo ya jamii.
  • Uelewa thabiti wa utawala bora wa maliasili, uhifadhi unaoongozwa na jamii, sera za mazingira, sheria, kanuni, na misingi ya kitaasisi nchini Tanzania.
  • Ujuzi wa vitendo wa uwezo wa kuandika maandiko ya miradi (proposals), mbinu za utafiti, na ushirikishwaji.
  • Historia iliyothibitishwa ya kufanikiwa kutumia na kuanzisha kadi za matokeo (scorecards), usimamizi unaolenga matokeo (RBM), na mbinu za utawala bora ili kuhakikisha utekelezaji bora wa miradi tata inayofadhiliwa na wafadhili katika nchi zinazoendelea.
  • Ujuzi wa kompyuta na uwezo wa kutumia programu za uchambuzi wa data (SPSS), Word, Excel, PowerPoint, Outlook n.k.
  • Uwezo wa kutumia vifaa na zana za kidijitali au za mkononi za kukusanya data kama vile Survey123.
  • Uwezo wa kufanya kazi chini ya shinikizo, kukidhi tarehe za mwisho za kazi, na kufanya kazi bila usimamizi wa karibu; uwezo wa kujihamasisha, kufanya kazi kwa ushirikiano, na ujuzi mzuri wa kuandaa taarifa na kutoa mada.
  • Ujuzi mzuri wa mawasiliano — ufasaha wa Kiswahili na Kiingereza, vyote kwa kuzungumza na kuandika. Nafasi hii inahusisha kufanya kazi na watu wa aina mbalimbali ndani ya taasisi, jamii za mitaa, na washirika wa ndani & wa kimataifa, ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wenzako wa kiufundi na wasio wa kiufundi.
Taratibu za Maombi

Maombi yote yawasilishwe pamoja na Barua ya Wasifu (CV/Resume) ya hivi karibuni, nakala za vyeti vya taaluma na matokeo (transcripts), hati za ushuhuda (testimonials), majina matatu ya wadhamini wanaoaminika, namba ya simu ya mchana au anwani ya barua pepe, na vitumwe kwa anwani ifuatayo ya barua pepe:

recruitment@janegoodall.or.tz

Ni waombaji pekee watakaochaguliwa kwenye orodha ya mwisho (shortlisted) ndio watakaohojiwa na kupewa marejesho ya usaili.

Mwisho wa Kutuma Maombi: Jumanne, Tarehe 22 Septemba 2026 kabla ya saa 11:00 jioni.

JGI Tanzania ni mwajiri anayetoa fursa sawa kwa wote na humchukulia kila mwombaji kwa msingi wa sifa bila kubagua rangi, asili ya kitaifa au ya kabila, imani ya dini, jinsia, na hali ya ndoa.

WAOMBAJI WANAWAKE WENYE SIFA PAMOJA NA WATU WENYE ULEMAVU WANAHAMASISHWA SANA KUOMBA.