Muhtasari wa Kazi
Kilimo ni moja ya visababishi vikuu vya kupotea na kuharibika kwa makazi ya sokwe, hasa pale ambapo uzalishaji mdogo, kilimo cha kuhamahama, na upanuzi wa mashamba vinapoongeza shinikizo kwenye maeneo yaliyosalia. Mtaalamu wa Kilimo (Agronomist) atasaidia kutatua changamoto hii kwa kutoa huduma za vitendo za kilimo, ushauri wa kiteknolojia, na huduma za ugani kwa wakulima ili kuongeza uzalishaji na ustahimilivu ndani ya maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kilimo kulingana na mipango ya matumizi ya ardhi iliyoidhinishwa, na hivyo kupunguza haja ya kukata misitu au kupanua mashamba kwenye makazi ya sokwe.
Nafasi hii itahamasisha kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi, kisichoharibu bioanuwai, na endelevu kinachoongeza mavuno, afya ya udongo, utunzaji wa maji, na maisha ya jamii huku kikipunguza shinikizo kwenye mifumo ya asili. Hii itajumuisha kuboresha uzalishaji wa mazao, rutuba ya udongo, udhibiti jumuishi wa wadudu na magonjwa, uboreshaji wa aina za mazao, kilimo mseto, na udhibiti wa mazao baada ya kuvuna pamoja na kuunganisha wakulima na masoko yenye bei nzuri. Mtaalamu atafanya kazi kwa karibu na wakulima, serikali za vijiji, watoa huduma za ugani, na timu za uhifadhi ili kuonyesha na kuunga mkono mbinu zinazofaa kijamii. Lengo kuu ni kutenganisha kukuza uzalishaji wa kilimo na upanuzi wa eneo la kilimo, kulikawezesha wakulima kuzalisha kwa njia endelevu kwenye maeneo yaliyopo huku wakichangia katika ulinzi na muunganiko wa makazi ya sokwe.
Majukumu na Kazi za Msingi
Majukumu kuu ya kiteknolojia yatajumuisha, lakini si tu:
-
Kupitia tafiti na maandiko yanayohusu mbinu bora za sasa katika sekta hii.
-
Kuhamasisha na kuwashirikisha wakulima kupitia viongozi wao wa serikali za mitaa ili kutumia mbinu zilizoboreshwa za kilimo (ikiwa ni pamoja na kilimo hifadhi na kilimo mseto) kinachochochea uendelevu.
-
Kushauriana na wakulima kuhusu mbinu za kilimo ili kuongeza kipato chao kutokana na mazao mbalimbali, na kwa ushirikiano na wadau wa sekta binafsi kupitia mifumo ya mikataba ya kilimo (out-grower schemes).
-
Kushauriana na wakulima pamoja na wasimamizi wa sheria kuhusu mbinu zitakazopelekea matumizi endelevu ya ardhi ya kilimo.
-
Kuanzisha na kusimamia mashamba darasa ili kutoa ushahidi wa kuonekana wa mafanikio ya mifumo tunayohamasisha.
-
Kutoa mafunzo kwa wakulima kulingana na mahitaji yaliyoainishwa hapo juu.
-
Kutathmini mwenendo wa mazao unavyoathiriwa na hali ya hewa, wadudu, na mbinu za usimamizi, na mara chache kutoa ushahidi kwa ajili ya bima.
-
Kufanya kazi kwa karibu na Afisa Misitu wa Programu na Afisa Mipango ya Matumizi ya Ardhi katika kubuni na kutekeleza mikakati ya usimamizi endelevu wa ardhi ya kilimo.
-
Kuandaa na kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa kazi kwa wakati.
-
Majukumu mengine yoyote utakayopangiwa na msimamizi wako au Uongozi.
Sifa za Chini za Kazi na Mahitaji Mengine
Sifa za chini za elimu na mahitaji mengine yatajumuisha, lakini si tu:
-
Stashahada (Diploma) au Shahada ya Kwanza (Bachelor's Degree) ya Kilimo (Agronomy/Agriculture) au fani inayohusiana kutoka chuo kinachotambulika.
-
Tajriba ya kazi ya angalau miaka 5 katika kutoa msaada wa kiteknolojia kwenye programu kubwa za kilimo.
-
Tajriba ya kufanya kazi katika maeneo ya vijijini na yaliyojitenga nchini Tanzania katika kutekeleza programu za usaidizi wa kilimo.
-
Tajriba ya kuwasaidia wakulima kutekeleza mbinu za kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi, ikiwa ni pamoja na mitindo ya kilimo biashara.
-
Tajriba ya kuimarisha mahusiano yenye usawa kati ya sekta binafsi, wadau wa kilimo, na wakulima wadogo.
-
Historia iliyothibitishwa ya kufanya kazi kwa mafanikio kwenye miradi tata inayofadhiliwa na wafadhili katika mazingira ya vijijini.
-
Ufahamu na tajriba ya awali katika kufanya kazi ya kuunga mkono miradi ya uhifadhi na usimamizi endelevu wa maliasili ni sifa ya ziada.
-
Ujuzi wa kompyuta na uwezo wa kutumia programu za uchambuzi wa data (SPSS), MS Word, Excel, PowerPoint, Outlook n.k.
-
Uwezo wa kufanya kazi chini ya shinikizo, kukidhi tarehe za mwisho za kazi, na kufanya kazi bila usimamizi wa karibu; uwezo wa kujihamasisha, kufanya kazi kwa ushirikiano, na ujuzi wa kuandaa taarifa na kutoa mada. Uwezo wa kukaa kwa muda mrefu katika mazingira ya vijijini.
-
Ujuzi mzuri wa mawasiliano - ufasaha wa Kiswahili na Kiingereza, vyote kwa kuzungumza na kuandika. Nafasi hii inahusisha kufanya kazi na watu wa aina mbalimbali ndani ya taasisi, jamii za mitaa, washirika wa ndani na wa kimataifa, pamoja na wafanyakazi wenzako wa kiufundi na wasio wa kiufundi.
Taratibu za Maombi
Maombi yote yawasilishwe pamoja na Barua ya Wasifu (CV/Resume) ya hivi karibuni, nakala za vyeti vya taaluma na matokeo (transcripts), hati za ushuhuda (testimonials), majina matatu ya wadhamini wanaoaminika, namba ya simu ya mchana au anwani ya barua pepe, na vitumwe kwa anwani ifuatayo ya barua pepe:
recruitment@janegoodall.or.tz
Ni waombaji pekee watakaochaguliwa kwenye orodha ya mwisho (shortlisted) ndio watakaohojiwa na kupewa marejesho ya usaili.
Mwisho wa Kutuma Maombi: Jumanne, Tarehe 22 Septemba 2026 kabla ya saa 11:00 jioni.
JGI Tanzania ni mwajiri anayetoa fursa sawa kwa wote na humchukulia kila mwombaji kwa msingi wa sifa bila kubagua rangi, asili ya kitaifa au ya kabila, imani ya dini, jinsia, na hali ya ndoa.
WAOMBAJI WANAWAKE WENYE SIFA PAMOJA NA WATU WENYE ULEMAVU WANAHAMASISHWA SANA KUOMBA.